FAHAMU MAJUKUMU YAKO
KWA NINI TUWE NA NGAZI YA MTAA
Kanisa la waadventista wa Sabato linazo ngazi rasmi nne za uongozi; (1) Kanisa mahalia (2) Conference/Field (3) Union Conference/Union Mission na (4) General Conference. Lakini ili kurahisisha utendaji ngazi mbili za Mtaa na Division ziliongezwa. Kusudi la msingi la kuwepo ngazi ya mtaa ni kurahisisha mawasiliano na kurahisisha ukuaji wa kitakwimu na wa kiroho wa makanisa yanayounda mtaa ili ifikie mahali mchungaji mmoja awe anachunga kanisa moja.
MAMLAKA YA MTAA
Baraza la mtaa linaloundwa na viongozi kadhaa wa makanisa na wale waliochaguliwa na mtaa hutoa maagizo na mapendekezo kwa makanisa yanayounda mtaa kuhusiana na maswala yenye maslahi na makanisa hayo kufuatia majadiliano yaliyohitimishwa na kura kutoka kwa wajumbe wa makanisa yote ya mtaa, walioketi katika baraza halali la mtaa. Makanisa kwa kutambua walituma wawakilishi katika baraza la mtaa hayatarajiwi kutotambua maamuzi ya mtaa ila yanaweza kuhitaji kuyaboresha zaidi maoni mapendekezo na maamuzi ya baraza hilo kwa roho ya masikilizano yenye lengo la kuhifadhi umoja.
MSAIDIZI WA MCHUNGAJI WA MTAA
- Atasaini barua zote zinazomhusu mchungaji wa mtaa anapokuwa hayupo na kuendesha majukumu yote ya kichungaji isipokuwa kubatiza na kufungisha ndoa.
- Atawasiliana na ofisi ya konferensi kupata mchungaji wa kuendesha huduma ya ubatizo na ndoa kwa agizo la mchungaji au mchungaji anapokuwa hayupo.
- Atapokea wageni wote wa mtaa na kuwapatia huduma zote zitakazohitajika kwa niaba ya mchungaji wakati mchungaji anapokuwa hayupo.
- Ataendesha vikao vya mtaa mchungaji asipokuwepo au anapoagizwa kufanya hivyo na mchungaji.
- Atasaidiana na katibu wa mtaa kuhakikisha fedha ya matumizi ya ofisi ya mchungaji inapatikana kwa wakati na kazi zilizokusudiwa hazikwami.
- Atasaidiana na katibu wa mtaa kuhakikisha taarifa za kila mwezi na kila robo zinaandaliwa na kutumwa konferensi kwa wakati.
- Atasaidiana na mkuu wa kambi na katibu wa mtaa kuhakikisha kamati za kambi zinatimiza wajibu wake na kuona kambi linafanyika kwa utulivu na mafanikio makubwa.
KATIBU WA MTAA
- Atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli za siku kwa siku za mtaa akishauriana na mchungaji wa mtaa ama msaidizi wa mchungaji anapokuwa hayupo.
- Atahakikisha ofisi ya mtaa inakidhi viwango wakati wote kwa kutunza nyaraka nyeti za kiofisi na vitendea kazi muhimu ili kutokwamisha huduma zozote za kiofisi.
- Ataandika minute za vikao vya mtaa na kuwapa taarifa wajumbe juu ya kuwepo kwa kikao cha mtaa na ajenda zitakazojadiliwa.
- Atatunza kumbukumbu za vikao na nakala za barua nyingine za mtaa kutoka katika ngazi za juu na zile zilizotumwa makanisani.
- Ataandaa fomu za taarifa zote za wakuu wa idara zinazohitajika kila mwezi na kila robo na kuzigawa kwa wahusika na kuwasaidia wale wasioelewa namna ya kuzijaza.
- Atahimiza utumaji wa taarifa za mwezi na za robo kwa wakati kutoka kwa wakuu wa idara ama kutoka kwa wakuu wa huduma wa makanisa ya mtaa.
- Atatoa ratiba ya utumaji wa taarifa za kila mwezi kwenye ofisi ya mtaa na kuwahimiza wahusika kuizingatia.
- Atapokea na kukagua taarifa ziendazo konferensi na kukatia risiti taarifa za fedha baada ya kuridhika nazo.
- Ataandaa taarifa ya fedha ya pamoja ya mtaa na kutuma Soft copy yake konferensi, mapema kabla ya siku ya kutuma taarifa.
- Atatunza nakala za taarifa za mtaa zinazotumwa konferensi kwa mwezi na kwa robo.
- Atasimamia makundi ya Whatsap ya mtaa na kuthibiti matumizi yasiyo sahihi.
- Atatoa matangazo ya mara kwa mara kwa wadau wote, kwa kadri yatakavyohitajika, na kwa kadri atakavyokuwa akiyapokea kutoka kwa mchungaji.
MKUU WA HUDUMA WA MTAA
- Atasaidiana na wakuu wa idara kuhimiza ujazwaji wa taarifa kwa usahihi na kwa wakati na kuhakikisha kuwa taarifa hizo zimemfikia mchungaji au katibu wa mtaa kwa wakati.
- Atahimiza wakuu wa Huduma kusimamia magoli yao waliyopewa na mtaa na kushauri namna bora ya kufanikisha mipango ya uongoaji wa roho waliyonayo.
- Kuratibu semina ya watenda kazi wa nyumba kwa nyumba na wa mahubiri ya hadhara ili kuwa na hazina ya kutosha kwa matumizi ya mtaa na makanisa mahalia.
- Kusimamia mkakati wa uongoaji wa roho wa kimtaa uliopo, na kupendekeza bajeti husika, na kamati mbalimbali za mkakati huo.
- kuunganisha mapendekezo ya bajeti za kamati mbalimbali za makambi, na kushauriana na mchungaji na katibu wa mtaa juu namna bora ya kufanikisha makambi hayo.
- Ataratibu ratiba ya wahubiri wa mtaa watakaokuwa wakitoa huduma makanisani kwa mzunguko war obo, akisaidiana na mchungaji na katibu wa mtaa.
MRATIBU WA MUZIKI
- Kuratibu vikundi vya uimbaji katika mikusanyiko inayofanyika kimtaa.
- Kuratibu makongamano ya kwaya na makongamano ya vikundi vya uimbaji kimtaa kwa lengo la uinjilisti, kusifu, na kujinoa kitaaluma.
- Kuratibu mafunzo ya utaalam wa muziki kwa waalimu wa kwaya, wahudumu wa nyimbo za vitabuni, wanakwaya na waimbaji kutoka vikundi vya uimbaji.
- Kuratibu Mass choir ya mtaa katika matukio ya kimtaa.
MRATIBU WA HUDUMA ZA WANAWAKE
- Kuratibu na kuhamasisha ushiriki wa wanawake wa mtaa katika semina, makongamano ya kimtaa,na ya ngazi za juu.
- Kuratibu na kuandaa mafunzo ya wanawake wa mtaa kwa kuwaalika wawezeshaji mbalimbali waliobobea katika fani na taaluma zenye changamoto kwa wanawake.
- Kusaidia kuitambulisha huduma ya wanawake makanisani ili kuongeza uelewa na uungwaji mkono wa huduma hii.
- Kuratibu namna ya kusaidia wanawake wenye changamoto na watu wengine wenye mahitaji maalum walio kwenye jamii tunayoishi.
- Kuratibu mkutano wa injili utakaoendeshwa na wanawake ili kuimarisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za ushuhudiaji na uongoaji wa roho.
KIONGOZI WA MAJENGO
- Kusimamia miradi yote ya ujenzi ya kimtaa na kuikamilisha kwa wakati.
- Kupendekeza bajeti ya miradi mbalimbali ya ujenzi ya kimtaa na kuiwasilisha kwenye vikao vya mtaa husika.
- Kwa kutumia kamati ya ujenzi ya mtaa atakayoiunda na kwa ushawishi wake, atatafuta wafadhili wa ndani na nje wa kusaidia kukamilisha miradi ya ujenzi ya mtaa iliyopo na inayokusudiwa kuzinduliwa.
- Kuhimiza upatikanaji wa hati za viwanja vya makanisa ya mtaa.
- Kushirikisha washiriki waliopo kwenye nafasi za utoaji maamuzi wa migogoro ya ardhi, ili kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa viwanja vyenye migogoro.
- Kusaidia upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kwa gharama nafuu kupitia msamaha wa kodi, na punguzo la bei kutoka kiwandani.
MRATIBU WA WATOTO NA VIJANA
- Kuratibu mikutano ya injili ya kimtaa, inayoendeshwa na vijana na watoto
- Kuratibu mafunzo ya wahubiri vijana na watoto kwa kutumia wakufunzi wabobezi.
- Kuhimiza kuhudhuria mikutano na makongamano yaliyoitishwa na ngazi za juu
- Kuratibu makongamano na mikutano ya vijana na watoto ya mtaa.
- Kuratibu matendo ya huruma ya kimtaa.
- Kusaidia kuinua kanisa lililo nyuma katika shuguli za vijana na watoto.
MRATIBU WA SHULE YA SABATO
- Kuratibu Shule ya Sabato inayohitimisha makambi ya mtaa.
- Kuratibu Shule ya Sabato kwenye tukio la ibada ya pamoja ya mtaa.
- Kuratibu semina ya mtaa ya viongozi wa shule ya Sabato.
- Kwa kusaidiana na kiongozi wa mtaa wa watoto, kupendekeza waalimu wa watoto watakaohudumu katika makambi ya mtaa.
- Kuratibu semina ya uendeshaji wa vipindi vya majadiliano ya lesoni redioni.
- Kuhimiza makanisa na washiriki kushiriki katika kuendesha mijadala ya lesoni redioni.